We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, August 17, 2019

Tanzania Yamwagiwa SIFA Kwa Kuwa Nchi Pekee ya SADC Ambayo Uchumi Wake Unakua Kwa Asilimia 7

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya SADC  Dr. Stergomena Lawrence Tax ameipongeza Tanzania kuwa nchi pekee ambayo imeongoza kwa kukidhi vigezo vya ukuaji wa uchumi, kwa kufikia asilimia 7, ikiwa ni tofauti na nchi nyingine.

Kauli hiyo ametoa wakati wa mkutano wa kwanza wa SADC uliofanyika jijini Dar es salaam, ambapo viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo wakiwemo viongozi wastaafu na Mawaziri wamehudhuria.

Dk.Tax amesema kwa nchi za jumuiya hiyo pamoja na mambo mengine kwenye eneo la uchumi kuna malengo ambayo yamewekwa kwa nchi wanachama na Tanzania ni nchi pekee ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia saba na hivyo wanastahili kupongezwa.

 "Uhimilivu wa uchumi ni nyenzo muhimu katika maendeleo, nchi wanachama zimekidhi vigezo vya SADC kiuchumi, takwimu zimeonesha Tanzania inafanya vizuri, na kwa vigezo pekee Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo imefikia ukuaji wa asilimia 7, mjipongeze." Amesema Dr Tax na kuongeza;
 

"Katika kufikia uchumi wa Viwanda nchi wanachama hawana budi kukuza uzalishaji wa umeme, kwa kuwa ni kitu muhimu kwenye ujenzi wa viwanda, nashukuru katika wiki ya Viwanda  hata Tanzania ,  tumeona mradi mkubwa wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji ambao ujenzi wake unaendelea"

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list