Simba imeanza vyema kutetea ubingwa wake baada ya kuifumua JKT Tanzania mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam
Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi ni ilihesabu bao mapema kwenye dakika ya kwanza likifungwa na mfungaji bora wa msimu uliopita Meddie Kagere
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems, aliwaanzisha wachezaji wapya wanne kwenye kikosi chake Tairone Dos Santos, Gerson Fraga, Deo Kanda na Haruna Shamte
Simba iliyotawala mchezo huo kwa muda mwingi, ilifunga mabao mengine mawili kwenye kipindi cha pili kupitia kwa 'Terminator' Kagere na Miraji Athumani
Kagere angeweza kuondoka na mpira leo kama shuti alilopiga nje kidogo ya 18 lisingegonga mtambaa panya kwenye moja ya majaribio aliyofanya langoni kwa JKT
Bao la kufutia machozi kwa upande wa JKT lilifungwa na Edward Songo kwenye dakika ya 87 kwa shuti la nje ya 18
Ushindi huo wa leo umerejesha furaha ya mashabiki waliokuwa na huzuni baada ya timu yao kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa mwishoni mwa wiki
Aidha ni mwanzo mzuri kwa Simba, matokeo haya ni ujumbe kwa timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom.

No comments:
Post a Comment