We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, August 5, 2019

Simba mmemsikia Mkuchika?


MASHABIKI wa Simba ambao wanajiandaa kwa ajili ya Tamasha la Simba Day, huenda wasioifurahie taarifa hii iliyotolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Yanga, Kapteni George Mkuchika.


Waziri huyo wa Serikali ya Awamu hii ya Tano, amesema  kwa mziki uliopo Jangwani kwa sasa, ubingwa lazima urejee Yanga baada ya misimu miwili watani wao Simba kulibeba wakiwapora msimu wa 2017-2018.

Mkuchika amekiri safari hii Yanga wana timu tishio na inapiga soka la kitabuni hivyo haoni kama kuna timu itagusa moto wao.
Mwenyekiti huyo alikuwepo uwanjani jana huku akiridhika na matokeo ya sare ya bao 1-1 iliyopata timu yake dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya.

Amesema licha ya kwamba matokeo yalikuwa sare lakini ameridhika na kiwango kikubwa kilichoonyeshwa na wachezaji wa Yanga huku wakimiliki mpira kwa vipindi vyote viwili.
"Tulimiliki mpira sehemu kubwa ya mchezo,wachezaji wamecheza vizuri sana ndio maana unaona licha ya sare lakini mashabiki wameridhika na soka waliloliona.

Alisema wanajivunia mwaka huu timu wanayo na wapinzani watapata tabu sana na wale waliochukua ubingwa msimu uliopita wanatakiwa kuwapisha kwani wenye nafasi yao wanarudi msimu huu.
"Tunashiriki ligi kwa sababbu tunataka ubingwa na tumezoea kuwa mabingwa kwani hata ukiangalia wapinzani wetu wakubwa ambao tunashindana nao kwenye mbio za ubingwa hawatufikii kwa kuwa sisi tumechukua Kombe mara nyingi"alisema Mkuchika.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list