Katika mwendelezo wa Sportpesa Simba Week, leo klabu ya Simba itakuwa na zoezi la uchangiaji damu kwa kushirikiana na mpango wa Taifa wa damu salama
Zoezi la uchangiaji damu ambalo limedhaminiwa na Taasisi ya Mo Dewji, leo litafanyika maeneo ya Stendi ya Mbagala na Ubungo
Wapenzi, wanachama na mashabiki wa Simba wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo
Siku ya kesho Jumamosi zoezi litafanyika Makao Makuu ya klabu, Msimbazi Kariakoo na Stendi ya Mbagala
Muda ni kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa 11 jioni

No comments:
Post a Comment