We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, August 30, 2019

Serikali kuanza kuwachukuliwa hatua wanaosambaza taarifa za uongo kuhusu dawa

Serikali ya Tanzania ipo mbioni kuanza kuwachukulia hatua wanaosambaza katika mitandao ya kijamii taarifa za uongo kuhusu madhara anayoweza kuyapata mtu iwapo atatumia aina flani ya dawa.
Hayo yamesemwa jana Alhamisi Agosti 29, 2019 na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Ofisi za Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) akiongozana na kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Amesema kuwa dawa zinazouzwa nchini huthibitishwa ubora wake na TMDA kabla ya kuuzwa na hakuna dawa iliyo bora zaidi ya nyingine.
”Niwaombe wananchi kutosambaza taarifa ambazo hawana uhakika nazo, kama wana swali au hoja kuhusu ubora wa dawa ni bora wawasiliane na TMDA kwa sababu sasa tutaanza kuchukulia hatua kwa upotoshaji usio na msingi,” amesema Dkt. Ndugulile.
Aidha, amesema kuwa wananchi hawapaswi kuwa na mashaka na dawa zinazouzwa katika maduka kwasababu maabara ya TMDA inaongoza kwa ubora Barani Afrika na wapo katika mkakati wa kuomba kibali cha kutambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
“Tukipata kibali majibu ya vipimo tutakayokuwa tunayatoa Tanzania yatakuwa yanakubalika dunia nzima na itakuwa ni hatua kubwa kwetu,” amesema Dkt. Ndugulile.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list