Rais Magufuli jana August 29, 2019 ametaja sababu inayosababisha usimamizi mbaya wa rasilimali za Bara la Afrika kuwa ni tafsiri potofu ya msingi wa maendeleo kwa kudhani fedha ni msingi wa maendeleo hali iliyosababisha viongozi wake kuzunguka katika Mataifa tajiri kuomba misaada na mikopo ambayo inawezekana inatokana na rasilimali za Afrika.
JPM amewataka kuelekeza nguvu katika kusimamia na kutumia rasilimali zilizopo huku akisisitiza maneno ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyesema ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.
No comments:
Post a Comment