Rais wa Uganda Yoweri Museveni, anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania mapema mwa mwezi Septemba, ambapo atakutana na kufanya majadiliano ya fursa za uwekezaji miongoni mwa nchi hizo mbili na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 30 jijini Dar es Salaam na Balozi wa Uganda nchini Richard Kabonero ambaye ameelza kuwa Rais Museveni anatarajiwa kuwasili nchini siku ya Septemba 6, 2019.
Aidha ameeleza kuwa kabla ya ziara hiyo kutakuwepo na ujio wa wafanyabiashara zaidi ya 300 kutoka nchini humo kuhudhuria jukwaa la biashara baina ya wawekezaji wa Tanzania na Uganda.
''Wiki ijayo kutakuwa na mkutano mkubwa hapa Rais wetu atakutana na Rais mwenzake Rais Magufuli, kuhusu wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda, tuko na waganda kama 300 watakuja'' amesema Balozi Kabonero.
Balozi Kabonero amesisitiza kuwa, majadiliano hayo ndiyo mwanzo wa mkakati wa ushirikiano wa kuboresha mahusiano ya kimaendeleo, katika sekta mbalimbali ikiwemo usafiri wa anga.
No comments:
Post a Comment