Mkazi wa Kijiji cha Kagera wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, Celestin Masatu (39) amefariki dunia baada ya kujichoma na kisu na kisha kujikata koromeo, ikiwa ni saa chache tu baada ya kumchomachoma mke wake na kisu mwilini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro amesema kuwa, tukio hilo lilitokea Agosti 28 majira ya usiku katika nyumba ya kulala wageni iliyoko Nakatungulu, Nansio Ukerewe, ambapo baada ya kukaguliwa kwenye baadhi ya vitu walivyokuwa navyo alikutana na ujumbe unaosadikika kuwa ni wa marehemu, ukimuomba msamaha Rais Magufuli kwa kitendo alichokifanya.
"Sehemu ya barua hiyo imeandikwa hivi, 'Naomba radhi kwa serikali inayoongozwa na Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kitendo nilichofanya kwa hiari yangu'' amesema RPC Muliro.
Kamanda Muliro amesema kuwa, kabla ya mwanaume huyo kujidhuru mwenyewe, alimchoma visu tumboni na shingoni mkewe na kusababisha utumbo na mfuko wa kizazi uliokuwa na mtoto mchanga wa miezi miwili kutoka nje, ambapo wote kwa pamoja walikimbizwa hospitalini na mwanaume huyo alifariki siku ya jana ya Agosti 29 na mke wake alihamishiwa hospitali ya Bugando.
No comments:
Post a Comment