We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, August 30, 2019

Rais Magufuli ataja tatizo la viongozi Afrika

Rais John Pombe Magufuli, ametoa wito kwa Mataifa ya Afrika kutafsiri vizuri dhana ya uhuru na kujiepusha na masalia ya fikra za kikoloni za kuamini watawala wa zamani wa Afrika ndiyo wenye uwezo wa kusaidia kuendeleza rasilimali za Afrika.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo  leo 29 Agosti, 2019 Ikulu Jijini Dar es salaam, alipokuwa akihutubia mkutano wa 6 wa Jukwaa la Uongozi Afrika unaohudhuriwa na Marais Wastaafu, Benjamin William Mkapa, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Thabo Mbeki (Afrika Kusini) na Hassan Mohamud (Somalia).
Maana hasa ya kupigania uhuru ilikuwa ni kurejesha rasilimali na hasa maliasili zetu, lakini pia kuwa na maamuzi kamili kuhusu namna ya kuzisimamia na kuzitumia kwa manufaa yetu, ili kuleta ukombozi wa kiuchumi, na hii ndio maana pekee ya kulinda uhuru wa kisiasa." amesema Rais Magufuli.
"Tusijidanganye watawala wetu wa zamani hawawezi kugeuka kwa usiku mmoja na kuwa wajomba zetu au wakombozi wetu kiuchumi, utegemezi huu ndio umeimarisha mizizi na misingi ya ukoloni mamboleo, ni lazima tuamke” amesisitiza Rais Magufuli.
Aidha ametaja sababu ya pili inayosababisha usimamizi mbaya wa rasilimali za Bara la Afrika, kuwa ni tafsiri potofu ya msingi wa maendeleo, kwa kudhani fedha ni msingi wa maendeleo hali iliyosababisha viongozi wake kuzunguka katika Mataifa tajiri kuomba misaada na mikopo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list