Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Brnabas Mwakalukwa, amesema kuwa mtoto aliyeangukiwa na bomba kubwa la maji mkoani humo, amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Bugando kwa ajili ya matibabu.
Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya msingi Kiyungi iliyopo Manispaa ya Tabora, alipata majeraha siku ya Agosti 28 baada ya kuangukiwa na bomba kubwa la kupitisha maji, walipokuwa wakicheza na wenzao hali iliyopelekea mtoto mwenzake kufariki muda huo huo.
''Yule mtoto aliyelazwa ICU walifanya utaratibu wa kumpeleka Bugando lakini bahati mbaya akafariki njiani maeneo ya Nzega, na daktari akathibitisha kufariki kwake'' amesema ACP Mwakalukwa.
Mabomba yaliyosababisha madhira hayo ni ya mradi mpya wa usambazaji wa maji mkoani humo kutoka Ziwa Victoria, yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye kiwanja cha shule hiyo.
No comments:
Post a Comment