Jalada la kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara, Abdul Nsembo na mkewe, Shamim Mwasha bado linachapishwa.
Akiongea leo Ijumaa Agosti 30, 2019 mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon amesema kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.
Wakili Simon amesema wamepewa taarifa na polisi kuwa jalada la kesi hiyo linaendelea kuchapishwa na wanasubiri majibu ya kielelezo kutoka kwa mkemia mkuu wa Serikali ambacho ni dawa ya kulevya aina ya Heroin.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba, 2019 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande.
Shamimu na mumewe walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani mnamo Mei 13, 2019 wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.
No comments:
Post a Comment