Msaidizi binafsi wa rais wa Marekani Donald Trump amelazimishwa kujiuzulu kutoka White House baada ya kujulikana kimakosa kwa taarifa zinazo ihusu familia ya Trump
Madeleine Westerhout, mwenye umri wa miaka 29, aliondolewa kazini ghafla siku ya Alhamisi baada ya rais kubaini kuwa amekuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa chakula cha jioni mwezi huu .
Alikuwa akinywa pombe na kujisifu kuhusu namna anavyoweza kumfikia rais Trump wakati wa mapumziko ya New Jersey, kimeripoti kituo cha habari cha CBS News
Bi Westerhout alifanya kazi na Trump tangu siku yake ya kwanza ya urais. Ikulu ya White House imekataa kutoa kauli yoyote juu ya kufutwa kazi kwake.
Gazeti la New York Times, ambalo liliripoti kwa mara ya kwanza juu ya kufutwa kazi kwa Westerhout, lilisema kuwa chanzo cha habari cha White House alisema kwa sasa anachukuliwa kama “mfanyakazi aliyetengwa ” na kwamba atazuiwa kurejea katika ikulu hiyo Ijumaa.Bi Westerhout akionekana katika mazungumzo na mkuu wa wafanyakazi wa zamani wa White Hous John Kelly
Akielezewa na vyombo vya habari vya Marekani kama mlinzi wa lango la Trump , Bi Westerhout alikuwa na ofisi yake mkabala na ofisi ya rais inayofahamika kama Oval Office katika jengo la West Wing.
Kauli zake anazoshutumiwa kuzitoa kwa wandishi wa habari alizitoa wakati wa chakula cha jioni na hazikuwa zinarekodiwa wakati alipokuwa akizungumza na maripota katika hoteli ya Berkeley Heights, New Jersey, wakati Bwana Trump alipokuwa mapunzikoni katika klabu yake iliyopo Bedminster, New Jersey, mapema mwezi Agosti.
Vyanzo vya habari vimeiambia CBS News kuwa alikuwa akinywa pombe na akatoa taarifa kuihusu familia ya rais. Pia ameripotiwa kutoa taarifa za uvumi kuwahusu watangazaji wanaotaka kumuona rais.
Mpaka sasa haijafahamika ni vipi Trump alifahamu mazungumzo hayo yote.Bi Westerhout akiwa katika Trump Tower
Maafisa kadhaa wa Ikulu ya White House kwa muda mrefu walishuku kuwa Bi Westerhout hamuheshimu Bwana Trump, huku mmoja wa maafisa wa zamani akiiambia CBS kuwa : ” Alikuwa jasusi kuanzia siku ya kwanza ambaye alitaka kutumia ukaribu wake kwa rais kuwanufaisha wapinzani wake”
Kwa mujibu wa vitabu viwili vilivyoandikwa kuhusu Trump katika White House, Bi Westerhout, ambaye alikuwa msaidizi wa zamani wa kamati ya Taifa ya Republican , alikasirishwa na kuonekana akilia katika usiku wa uchaguzi ilipojulikana wazi kuwa Trump alikuwa ameshinda.
Licha ya kutofurahishwa kwake na ushindi wa Bwana Trump, alifanikiwa kupata kazi ya usaidizi wa Trump inayoripotiwa kumlipa $145,000.
Wakati wa kipindi cha mpito cha Bwana Trump, Bi Westerhout mara kwa mara alikuwa akiwasindikiza wageni katika ofisi ya Trump Tower iliyopo New York.Madeleine Westerhout akiwa amesimama mbele ya ofisi ya Oval mwaka jana
Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, alikuwa na ukurasa wake binafsi wa Instagram ambapo alituma jumbe na picha kuhusu maisha yake katika White House na safari alizokuwa akizifanya na rais.
Katika ujumbe mmoja alitania juu ya namna alivyolazimika kuchapisha kipande cha karatasi ambacho Trump alikuwa amekishikilia katika tukio la umma.
Wakati mwandishi wa habari wa siku nyingi Bob Woodward alipolalamika kwamba ombi lake la kuzungumza na Bwana Trump katika mahojiano halikufikishwa na wasaidizi wake wa ngazi ya juu kama Kellyanne Conway, Bwana Trump alisema angepaswa kuongea na Bi Westerhout.
“Madeleine ni mtu muhimu. Ni mtu anayeweza kutunza siri ,” Alisema Bwana Trump.
Kwa mujibu wa CBS, Bwana Trump amekuwa akimuelezea mara nyingi kama “mrembo wangu”.
No comments:
Post a Comment