Baada ya Simba SC kuondolewa na UD Songo ya Msumbiji katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 1-1 uwanja wa Taifa (agg 1-1), muwekezaji wa Simba SC MO Dewji ameeleza kwa kina kuhusiana na alivyoyapokea matokeo hayo na wanasimba wasione tu yupo kimya.
“Wanasimba, mnisamehe kwa ukimya. Maumivu ya matokeo yametupata sote. Naomba tukumbushane: Sisi ni SIMBA! Simba lazima anyanyuke! Hawezi kukata tamaa, Niwaombe tusivunjike moyo wala kukata tamaa”>>> MO Dewji
“Hatutaogopa maneno ya watu na hatutaacha kupambana na kujipanga kwa ajili ya malengo yetu. Msimu huu tutautumia kikamilifu kuhakikisha tunaboresha mipango yetu ili msimu ujao turudishe furaha kwa Wanasimba wote, Tumwombe Mwenyezi Mungu atutangulie katika safari yetu endelevu. Tukumbushane tena: Roma haikujengwa kwa siku moja. Tuwe wavumilivu, tutafika tu Insha’Allah. 🙏🏽”>>> MO Dewji
No comments:
Post a Comment