Hali hiyo iliwafanya wananchi kuamini kuna ndege imeanguka, kuchochewa zaidi na magari ya kikosi hicho yaliyokuwa yakielekea na kutoka katika uwanja huo, yakiwa yamepakia watu waliokuwa wakiigiza kama majeruhi waliokuwa wakipelekwa hospitali.
Evarista Mutasingwa wamesema aliamini ni tukio la kweli baada ya ulinzi mkali kuimarishwa na magari ya usalama kuongezeka.
Zoezi hilo lililoshirikisha vikosi mbalimbali halikujulikana na limetajwa kama hatua ya kupima utayari iwapo litatokea tatizo linalohitaji kukabiliwa kwa mazingira ya dharura.
Akizungumza na Mwananchi kamanda wa kikosi hicho mkoani Kagera, Hamis Dawa amesema wamefika mapema kwenye eneo la tukio na kushiriki kuzima moto na shughuli za uokoaji.
Ametaja baadhi ya changamoto zilizobainika kuwa ni uchache wa magari ya kusafirisha wagonjwa na wataalamu wa afya katika hospitali walikopelekwa majeruhi wa ajali hiyo.

No comments:
Post a Comment