Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana ilishindwa kuendelea na ushahidi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, akiwemo mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, kutokana na wakili wa washtakiwa hao, Peter Kibatala kutokuwepo mahakamani.
Kibatala alitakiwa jana Ijumaa Agosti 30,2019 kumhoji shahidi wa saba katika kesi hiyo, Victoria Wihenge ambaye ni Ofisa Uchaguzi kutoka Manispaa ya Kinondoni, lakini hadi kesi hiyo inaahirishwa alikuwa hajatokea Mahakamani.
Uamuzi wa kuahirisha kesi hiyo ulitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 10, 11 na 12, 2019 itakapoendelea.
No comments:
Post a Comment