Shahidi huyo mjumbe wa Bodi ya Simba, Kassim Dewji alidai hayo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba huku akiongozwa na Wakiri wa Takukuru, Leonard Swai.
Dewji alidai kuwa wakati huo klabu hiyo ilikuwa na madeni mengi walikubaliana kwenye kikao cha kamati ya utendaji, kiasi cha Dola za Marekani 17,000 alipwe Zacharia Hanspope ambaye alikuwa anaidai klabu hiyo.
Alidai kuwa kiasi cha fedha kilichobakia ifunguliwe akaunti inayoitwa Bunju ili fedha hizo ziingizwe humo na baadae zitumike kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa uwanja cha mpira wa klabu hiyo.
Baada ya kufanyika kwa makubaliano hayo kuhusiana na fedha ziingizwe kwenye akaunti, jambo la utekelezaji waliachiwa watendaji akiwemo aliyekuwa Rais wa Klabu hiyo Evans Aveva na Amos aliyekuwa ni Kaimu Katibu na mweka hazina wa klabu.
"Watu hawa waliokuwa ndio wasimamizi wakuu wa mchakato mzima wa kufungua akaunti ya Bunju, hata hivyo baada ya makubalianao hayo kuhusu fedha, mimi sikudhuhuria kikao chochote cha kamati tendaji kwakuwa nilikuwa nasafiri mara kwa mara" alidai Dewji.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 4, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.Alidai fedha hizo zilizotakiwa kuwekwa kwenye akaunti kwa ajili ya ujenzi wa uwanja, ikiwemo kununua nyasi pamoja na kiasi kingine kitumike kumlipa mkandarasi.
Mbali na Aveva washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Godfrey Nyange (Kaburu) ambaye alikuwa Makamu pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zachariah Hans Pope.
Wanakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji wa fedha.
Katika shtaka la utakatishaji fedha linalomkabili Aveva, inadaiwa Machi 15,2016 katika benki ya Barclays Mikocheni, Dar es Salaam alijipatia Dola za Kimarekani 187,817, takriban Sh 400 milioni kutoka katika timu ya Simba wakati akijua zimetokana na zao la kosa la kughushi.
Katika shtaka la kughushi linawakabili washitakiwa wote, ambapo wanadaiwa katika tarehe hizo kwa pamoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya Sh90 milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.
Pia katika shtaka lingine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya Machi10 na Septemba 30, 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.

No comments:
Post a Comment