Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu, amesema Tanzania na Kenya kwa sasa zinatakiwa kuwekeza zaidi kwenye suala la elimu ili kuhakikisha mataifa haya yanapiga hatua zaidi kwenye suala la maendeleo.
Kazungu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye East Afrika Breakfast cha East Afrika Radio, juu ya uhusiano baina ya Kenya, Tanzania na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kazungu amesema kuwa, "Mkuu wa Sheria Kenya alikaa miaka 10, alikuwa mwanafunzi hapa Tanzania, hata mjomba wangu alikuwa mtu mkubwa Kenya alisoma hapa Tanzania, kwa hiyo kitu cha kwanza tunachopaswa kukitumia kama fursa ni kuangalia suala letu la elimu".
"Ningeomba watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa watu wa moja na lengo letu liwe moja, ni muhimu sana tunatakiwa kujua tunamajukumu makubwa zaidi kwenye Jumuiya, hatukatazwi kuzipenda nchi zetu lakini tujue tunajukumu kubwa zaidi kwenye Jumuiya yetu." amesema Kazungu.
Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipokea dhahabu na pesa taslimu ambazo zilikamatwa nchini Kenya zaidi ya miaka 10 iliyopita.
No comments:
Post a Comment