Aliyekuwa mlinzi wa kati wa Simba Juuko Murushid ameelekea Morocco kujiunga na Wydad Casablanca
Juuko anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo iliyocheza fainali ya ligi ya mabingwa msimu uliomalizika
Hivi karibuni Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori alisema Juuko alikuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na mabingwa hao wa Tanzania Bara
Hata hivyo Simba ilisitisha kumlipa mshahara baada ya kuondoka kambini kabla ya ligi kumalizika msimu uliopita
Juuko ni miongoni mwa wachezaji walioisaidia Uganda kutinga hatua ya mtoano michuano ya Afcon 2019 iliyomalizika mwezi uliopita nchini Misri

No comments:
Post a Comment