We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, August 3, 2019

GSM: Jezi za Yanga zipo nyingi tu


BAADA ya kuwepo taarifa kwamba jezi mpya za Yanga zimekwisha, Kampuni ya GSM ambayo imepewa tenda ya kusambaza jezi hizo imesema mzigo bado upo mwingi nchini na mwingine unaendelea kuingia kutoka nchini China.

Leo Jumamosi, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo walijazana makao makuu ya Yanga wakihitaji jezi hizo kwa ajili ya kuzivaa kesho Jumapili ambapo ndiyo kilele cha Wiki ya Wananchi lakini hawakuzikuta.

Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM, Hersi Said amewatoa hofu mashabiki wa Yanga kwamba wanaendelea kusambaza jezi hizo nchini hivyo zitapatikana sehemu mbalimbali ambazo wameziweka kwa ajili ya kuuza.

"Mzigo upo ila ulimalizika kwenye maeneo ambayo tulipeleka lakini limefanyiwa kazi na jezi zitapatikana, si hivyo tu kuna mzigo mwingine unaingia kwa kila ndege inayokuja kutoka China kwani hatukuweza kusafirisha kwa pamoja kutokana na muda pamoja na gharama za usafirishaji.
"Niwatoe hofu mashabiki wa Yanga kuhusu hilo, jezi watazipata ingawa hatukutarajia kama muitikio ungekuwa mkubwa namna hii, inaonyesha ni kiasi gani Yanga ina mashabiki wengi kutokana na mahitaji kuwa makubwa.

"Hizi jezi zinazouzwa ziliingia juzi (Alhamisi) usiku na pia tarehe ya uzunduzi na kilele cha Wiki ya Wananchi nazo zimekuwa karibu sana, hivyo hata usafirishaji ukawa changamoto kidogo ingawa hilo halizuii upatikanaji wa jezi mpya za Yanga," amesema Said

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list