Hayo ameyasema leo katika uzinduzi wa jezi mpya kwa klabu hiyo msimu mpya wa ligi mwaka 2019/20, ameupongeza uongozi kwa kufanya usajili kwa kufuata matakwa ya mwalimu na sio wao binafsi.
"Sio mtabiri lakini kwa hili lililofanya katika usajili msimu huu naamini na nategemea mataji mengi kutoka Yanga, viongozi hawajasajili kwa utashi wao wamesajili kwa kuingatia matakwa ya kocha na benchi la ufundi msimu huu wamefanya kazi kubwa sana," alisema na kuongeza;
"Wachezaji waliosajiliwa kutoka mataifa mbalimbali naamini watakuwa ni kichocheo kwa nyota wa ndani kunyanyua vipaji vyao kwa kuchukua mbinu kutoka kwa wageni na kwa lengo la kuimarisha kikosi cha timu ya taifa."
"Watu wa zamani nadhani wanamfahamu mtabiri Sheikh Yahya Hussein nami leo naomba kutabili kuwa naona mambo makubwa kutoka Yanga msimu ujao kutokana na usajili bora walioufanya nawatakia kila rakhel," aliongeza.
Tangu kuanza kwa Ligi ya Bara mwaka 1965, Yanga ndio vinara wa kubeba mataji ikiwa na 27, ikifuatiwa na Simba yenye mataji 20, huku Mtibwa Sugar ikishika nafasi ya tatu na mataji yao mawili.

No comments:
Post a Comment