We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, August 31, 2019

Mashabiki Yanga wamkera Ajib

Kiungo mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib ameeleza kutofurahishwa na baadhi ya mashabiki wa Yanga ambao wamekuwa wakimzungumza vibaya licha ya kuifanyia mema klabu hiyo misimu miwili aliyoitumikia
Ajib alirejea Simba msimu huu baada ya kumaliza mkataba Yanga. Kuondoka kwake Yanga kumewavuruga baadhi ya mashabiki wa timu hiyo aliyokuwa nahodha na mmoja wa watia saini wa akaunti iliyokuwa imeanzishwa kuichangia timu hiyo
Ajib amesema baadhi ya maneno ya mashabiki yanamfanya ajitume zaidi lakini wengine wanamkosea heshima licha ya mema aliyoifanyia Yanga
"Najua ni maneno ya mashabiki ambayo siku zote hawataki kukubaliana na hali ilivyo, lakini nashangaa kuona wananizungumzia kwa mabaya tu, wakati yapo mazuri niliyofanya," amesema
“Muda mwingine maneno yao yananipa nguvu ya kujituma mazoezini ili niweze kuipa matokeo bora Simba na kuwanyamazisha, lakini nakereka na kuumia sana na maneno yao wanayonizungumzia wakati niliishi nao vizuri”
"Mchezaji kutoka sehemu moja kwenda nyingine si kosa na kumzungumzia vibaya au kumhusisha na mambo ya kichonganishi si vizuri kwa sababu ipo siku naweza kurudi Yanga,  jambo zuri ni kukubaliana na uhalisia ulivyo"

CHADEMA yahisi kufanyiwa mchezo mchafu

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano  wa  CHADEMA Tumaini Makene,  amesema kuwa madiwani wa Halmashauri ya Ubungo hawajagomea mkutano wa baraza hilo  bali wamehisi kuna mchezo mchafu unaofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kwa kushindwa kumuapishwa Diwani wa viti maalumu.

Akizungumza leo Agosti 31 na EATV & EA Digital, Makene amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha anaondoa vikwazo na kumuapisha Diwani huyo,  kwani kwa kufanya hivyo atakuwa anakiuka maagizo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwani ndiyo iliyomteua Diwani huyo wa Viti Maalumu, Anna Kajigiri .
''Walitarajia katika kikao cha leo  kwa mujibu wa ratiba Anna Kajigiri ataapishwa kuwa sehemu ya baraza, sasa madiwani wenzake wanahisi kuna mchezo mchafu unafanyika kwenye ofisi ya Mkurugenzi, kutomuapisha tofauti na maelekezo ya NEC ambayo imemteua Anna Kajigiri kuwa Diwani halali wa Halmashauri ya Ubungo, kimsingi hawajagomea mkutano isipokuwa waameeleza wasiwasi wao dhidi ya uzembe wa ofisi ya Mkurugenzi kushindwa kumthibitisha mwenzao kuwa diwani'' amesema Makene.
Kufuatia hali hiyo CHADEMA  imemuomba Mkurugenzi huyo kumuapisha Diwani wao  na kwamba yeye kama Mtumishi wa Umma  si vyema kuweka mbele masuala ya kisiasa na kukiuka maagiza ya NEC, chombo ambacho kina mamlaka ya mwisho ya kumtangaza nani anafaa kuwa Diwani au Mbunge.

Hatutarudia makosa mechi dhidi ya ZESCO - Ngasa

Nahodha msaidizi wa Yanga Mrisho Ngasa amesema wanajiandaa kikamilifu kushinda mchezo wa nyumbani wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United ambao utapigwa Septemba 14 kwenye uwanja wa Taifa
Ngasa amesema hesabu zao ni kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa
Kwenye mchezo wa nyumbani hatua ya awali dhidi ya Township Rollers, Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 hivyo kulazimika kushinda ugenini na hatimaye kufanikiwa kutinga raundi ya kwanza
"Tunaanzia nyumbani, hatupaswi kufanya makosa kama ilivyokuwa mchezo dhidi ya Rollers, tunahitaji ushindi," amesema
"Ushindi wa nyumbani utatupungizia presha ya mchezo wa ugenini hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi"
"Tumejiwekea malengo ya kuingia hatua ya makundi. Lolote linaweza kutokea tukishaingia hatua hiyo"

Goodluck Gozbert awajibu wanaodai ngoma yake "Nibadilishe" sio gospel


Muimbaji wa muziki wa injili nchini Goodluck Gozbert amefungukza kuwa hakuandika wimbo wa "Nibadilishe" kwa ajili ya watu waliookoka.

Kiongea kwenye kipindi cha Bongo Fleva cha Clouds FM, Gozbert amesema, “SikuandikaNibadilidshe kwa ajili ya watu waliookoka.”  

“Wakati naandika Nibadilishe sikufanya kwa ajili ya watu ambao wapo tayari kwenda mbinguni, bali nilifanya kwa ajili ya watu ambao wanajua kila kitu kuhusu dini yake na wanajua kuhusu Mungu na kuna vitu wanashindwa kuvifanya vya kiimani na hawajui kwanini vinawashinda,” ameongeza.

Msanii huyo amesema hayo baada ya watu wengi wamekuwa wakizungumza kuwa wimbo huo haujakaa ki-gospel.

Moto Wateketeza Ghala la Kiwanda Arusha

Moto  mkubwa ambao chanzo chake hakijajulikana, umezuka na kuteketeza moja kati ya maghala matatu ya kuhifadhia pamba katika kiwanda cha Sunflag kilichopo mkoani Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shanna, amesema kuwa moto huo umeanza kuwaka kuanzia majira ya saa 7:00 mchana, ambapo hadi sasa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefanikiwa kuuzima moto huo.

“Bado hatujajua chanzo chake, maofisa wangu wanaendelea na uchunguzi,” amesema Shana

LIVE: TAZAMA TAARIFA YA HABARI YA TBC ONE

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

LIVE: TAZAMA TAARIFA YA HABARI YA ITV

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

LIVE: TAZAMA TAARIFA YA HABARI YA AZAM TV

BOnyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

Yanga yaajiri Mkurugenzi wa ufundi kutoka Uingereza

Kuelekea ya Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya pili dhidi ya Zesco, Mkurugenzi mpya wa ufundi wa klabu ya Yanga ambaye atatokea nchini Uingereza, anatarajia kuanza kazi rasmi leo.
Mkurugenzi huyo, aliyekuwa anafanya shughuli za soka nchini Uingereza ni Mtanzania, aliyezaliwa visiwani Zanzibar akiwa amebobea katika masuala ya ufundi na program za vijana.
Mmoja wa viongozi wa Kamati ya Utendaji wa Yanga  alisema tofauti na ufundi, wakurugenzi wengine watakaonza kazi leo ni wa Masoko, Fedha na Sheria.
Kiongozi huyo  alisema hawajaweka majina ya watu hao hadharani  kutokana na kuwa walikuwa bado katika ajira na waliakubaliana  leo  ndiyo wanaweza kuwaweka wazi wakati wanapoanza majukumu yao rasmi.
“Rasmi kesho (leo), Mkurugenzi wa Ufundi ataanza kazi, anatokea Uingereza lakini ni Mtanzania aliyezaliwa Zanzibar, mkurugenzi wa masoko, sheria na fedha.
Kamati ya Utendaji ya Yanga, inatarajia kukutana leo na hao waajiriwa, baada ya hapo majina na CV zao zitawekwa wazi, tulishindwa kufanya hivyo mapema kwa kuwa walikuwa bado katika ajira,”  kilisema chanzo.
Alieleza kuwa nafasi nyingine ikiwamo ya katibu, ofisa mtendaji mkuu na ofisa habari, zinaendelea kushughulikiwa na kamati husika

Jeshi la Polisi Latoa Onyo Kwa Watakaofanya Vurugu Wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mtaa

Jeshi la Polisi nchini limewatahadharisha wale wote watakaoleta vurugu wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa  na kusema watachukuliwa hatua kali za kisheria

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime, ambaye amesema kuwa watu wakifuata sheria chaguzi zote nchini zitabaki kuwa na amani.

“Wale ambao wanahisi watatingisha kiberiti kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa, sisi tumejipanga vizuri kukabiliana nao kwa nguvu zote kwa jinsi ambayo tutazidi kupokea nguvu toka kwao au ubishani toka kwao” amesema Misime.

Wanaoihujumu Serikali na Kusababisha Ndege ya Tanzania Kushikiliwa Afrika Kusini Kufunguliwa Mashitaka

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas amesema serikali itawafungulia kesi ya kuhujumu nchi watu wote watakaobainika kuihujumu serikali juu ya kukamatwa kwa ndege ya Tanzania nchini Afrika Kusini, pindi kesi iliyoplekea kukamatwa ndege hiyo itakapomalizika.

Akizungumza mjini Dodoma leo Jumamosi Dk Abbas amesema wapo Watanzania wanaishiriki kuihujumu Serikali  kuhusu ndege hiyo, kwamba kuna siku uhujumu huo utawasaidia.

“Wapo wazawa wanaofanya mawili matatu kuhujumu nchi lakini niwaeleze tusubiri kesi iishe huko Afrika Kusini, tutawafungulia kesi ya kuhujumu nchi yetu.”

“Hakuna Nabii katika historia ya Manabii aliyewahi kuaminiwa kwa asilimia 100, hivyo huwezi kukubaliwa na watu wote, hata hii ndege inayoshikiliwa ikija Tanzania ipo siku wanaochukia watatumia usafiri huo kwenda Afrika Kusini kama sio wao basi watoto wao,” amesema Dk Abbas.

Jana Mawakili wanaoiwakilisha Tanzania katika kesi ya kuzuiwa ndege hiyo waliitaka mahakama Kuu ya Afrika Kusini kutupilia mbali zuio la kuzuia ndege ya shirika hilo ya Airbus A220-300, wakisema ilitolewa kimakosa.

Msiwe na hofu, ndege itaachiwa - Serikali

“Ninachosema, ukamate ndege…ukamate chochote utakacho kamata…sisi bwana …no retreat no surrender,”- Msemaji wa serikali Dkt Hassan Abas akielezea imani ya serikali juu ya kuachiwa kwa Ndege ya ATCL inayoshikiliwa nchini Afrika kusini. Msikilize.

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

Waziri Lugola Awataka Maafisa Uhamiaji Kuepuka Rushwa na Kutokuwanyanyasa Wawekezaji Nchini

Na Felix Mwagara, Moshi (MOHA).
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewataka Maafisa Uhamiaji nchini, kuepuka rushwa na kutokuwanyanyasa wageni na hasa wawekezaji nchini.

Akizungumza katika kikao cha Maafisa Uhamiaji Waandamizi kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Uhamiaji (Trita), Mjini Moshi, leo, Lugola alisema wawekezaji ni watu muhimu katika maendeleo ya nchi, hivyo wanaposumbuliwa kwa kunyanyaswa bila sababu za msingi ni kuvunja misingi ya uadalifu.

Pia Waziri Lugola aliwataka maafisa hao waache kutoa PI (tangazo la kuondolewa mtu asiye raia nchini) zenye utata kwa maslahi binafsi bila kuzingatia athari ambazo nchi inazipata.

“Yapo malalamiko kwamba kuna wageni wanaingia nchini na kuwekeza kwa ubia na Watanzania, biashara inapokuwa inaendelea Watanzania huwazunguka wageni na kuwatengeneza mazingira ya kuwafukuza ili wapate fursa ya kumiliki hizo biashara na hapo ndipo Idara ya Uhamiaji hutumika, acheni hayo mambo kwa kuwa yanatuchafua kama taifa letu,” alisema Lugola.

Aliongeza kuwa, Rais John Magufuli anatafuta wawekezaji kwa nguvu na kuwahakikishia usalama wao na biashara zao lakini baadhi ya watumishi wa umma badala ya kusaidia jitihada hizi wao wanatumika kuwafukuza kwa dhuluma.

Alisema wageni hao wakishafukuzwa na wanaacha uwekezaji wao nchini ambao wanadhulumiwa huko waliko wanaisema nchi vibaya na kwa uzoefu huo wageni wengine hawawezi kuja nchini.

“Tujitathimini, tuzingatie sheria, kanuni, taratibu na miongozo yetu kwa kuzingatia maslahi ya taifa, pia nawasihi sana mumsaidie mheshimiwa Rais kutimiza ahadi zake kwa Watanzania ambazo amezitoa kupitia Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na ahadi zake nyingine mbalimbali ambazo amekuwa akiahidi na kuzitekeleza,” alisema Lugola.

Aidha, Waziri Lugola kabla ya kukifungua kikao hicho kilichojumuisha Maafisa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, alisema kikao hicho kitakuwa chachu ya kudumisha maadili ya kazi, nidhamu, utii, na ushirikiano katika maeneo yao ya kazi ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya Idara hiyo ya Upendo, Mshikamano, Uwajibikaji na Kukataa Rushwa.

“Ni imani yangu kuwa, mtaendelea kutekeleza majukumu yenu kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma katika utoaji wa huduma bora kwa Wananchi,” alisema Lugola.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, alisema kikao hicho zitatolewa mada mbalimbali zitakazowasilishwa kuhusu rushwa na Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018 ambazo ndio mwongozo wa utendaji kazi wa  Idara ya Uhamiaji.

“Kwa kuwa Idara yetu ya Uhamiaji inatoa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo pasipoti, vibali vya ukaazi, pasi pamoja na viza, hivyo kupitia kikao hiki tutazingatia kikamilifu mada hizo kwa kuwa zitatusaidia katika kutoa huduma bora kwa maslahi ya Idara yetu, Wizara na taifa kwa ujumla,” alisema Dkt. Makakala.

Sugu afunga ndoa na mpenzi wake,wabunge wampongeza

Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi 'Mr.II Sugu' leo tarehe 31/08, 2019, amefunga ndoa na mpenzi wake Happiness Msonga, katika kanisa Katoliki Ruanda Jijini Mbeya.

Mmoja wa watu maarufu na mwanasiasa ambaye ni mbunge wa jimbo la Mikumi Mh.Prof Jay amewapa pongezi kwa kupost picha na video katika mitandao ya kijamii ya Instgram na Twitter ambapo ameandika,
"Muda wa kanisani harusi ya Jongwee, Mbeya stand up , Hongereni sana kaka yangu @jongwe__ na Shemeji yetu Happiness msonga kwa kukamilisha ndoa yenu takatifu leo, Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu Awabariki zaidi na awasiamie kwenye Maisha yenu ya NDOA, AMEN"
Mr II Sugu kabla ya kufunga ndoa na mke wake huyu wa sasa alikuwa na mahusiano mfanyabiashara na muigizaji Faiza Ally na walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike.
Mbunge mwingine ambaye amempongeza Sugu ni Mbunge wa Mtama (CCM), Mh Nape Nnauye.

Hongera sana kaka! Karibu kwenye club! Maisha yako yana historia ya kusimulia/ your life has a story to tell!👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾

View image on Twitter

51 people are talking about this

Chameleone afunguka Harmonize kufuta sauti yake, ‘sipendi kukosewa heshima’

Mwanamuziki nguli kutoka Uganda, Jose Chameleone amefunguka ya moyoni kuhusu uamuzi wa Harmonize kumuondoa kwenye wimbo wa ‘Inabana’ na kumuweka Eddy Kenzo, akieleza kuwa huenda hakupenda alichoimba.
Akifunguka katika mahojiano maalum aliyofanya jana na mtangazaji mmoja nchini Uganda, mkongwe huyo alieleza jinsi walivyokutana na Harmonize katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya na kupanga kufanya kazi.
Amesema mkali huyo wa ‘Kwangwaru’ alimuomba kumshirikisha kwenye wimbo wake na yeye alikubali kwakuwa anapenda anavyoimba.
Ameeleza kuwa walibadilishana namba za simu na anuani za barua pepe kwakuwa walikuwa na haraka. Baada ya muda mfupi alitumiwa beat (mdundo) akarekodi sehemu yake na kuwasilisha kwa Harmonize.
Kwa mujibu wa mkali huyo wa ‘Tubonge’, kupishana kulianza baada ya kuwa anapigiwa simu na meneja wa Harmonize akipewa maelekezo kwa ajili ya kufanya video, lakini yeye aliendelea kusisitiza kuwa angependa kuwasiliana na mwanamuziki mwenzake moja kwa moja. Kwa bahati mbaya haikuwa hivyo.
“Ndiyo, Harmonize ni msanii mkali sana lakini hata mimi sio mwanamuziki wa bei chee na ni msanii mkali pia. Lakini pindi nilipoomba nizungumze na Harmonize nadhani alikuwa bize sana na tulikuwa tumeshamaliza kurekodi wimbo na kilichokuwa kimebaki ni kufanya video tu,” alisema Chameleone kwa lugha ya Kiganda na kutafsiriwa Kiingereza na ripota wa SnS aliyeko Kampala.
“Kwahiyo, nilijiondoa mwenyewe kutoka kwenye mradi huu. Sitaki vitu vya kuhangaika sana na sipendi kukosewa heshima. Kwa miaka yote hii nimefanya muziki na sina nilichobakiza kuonesha kuwa naweza. Hivyo, nikawaambia kama yote yakimalizika basi tutaendelea, lakini mimi sina tatizo kwakuwa wanaopiga kasia kwenye mtumbwi, mmoja akiwa mbele na mmoja nyuma wote wanaelekea sehemu moja,” aliongeza.
Hata hivyo, Chameleone alimtetea Eddy Kenzo kwa kushiriki kwenye wimbo huo akiwataka mashabiki wasimlaumu kwani yeye alifanya kazi yake na mwenye uamuzi juu ya wimbo huo ni Harmonize mwenyewe.
“Inawezekana alipenda Eddy Kenzo alivyoimba na labda hakupenda mimi nilivyoimba lakini yote kwa yote yeye ndiye mwenye uamuzi, hata akisema amshirikishe Justin Bieber ni uamuzi wake,” Chameleone anakaririwa.
Sokomoko lilizuka mtandaoni baada ya video ya ‘Inabana’ ya Harmonize kutoka rasmi akiwa ameshirikishwa Eddy Kenzo, wakati sehemu ya wimbo huo aliyoshirikishwa Chameleone iliyokuwa imevuja mtandaoni awali haisikiki tena.
Baada ya kushambuliwa kila kona na mashabiki mtandaoni, Eddy Kenzo aliamua kujitetea hadharani akieleza kuwa yeye pia alipata mshtuko baada ya wimbo huo kuachiwa, aliposikia kuwa Chameleone alikuwa ameshirikishwa awali.
Amesema aliamua kumuuliza Harmonize na alikiri kuwa awali alirekodi na Chameleone lakini kulitokea kutoelewana akaamua kubadili uamuzi.
Kenzo amesema hana hatia katika hilo kwani alifanya kazi bila kujua kilichokuwa kimefanyika awali na hakuwa na lengo la kumkosea heshima Chameleone.
Mdogo wake Chameleone, Weasel alikuwa mmoja kati ya wanamuziki wa Uganda waliomvaa Eddy Kenzo wakidai amemkosea heshima mkongwe huyo.



Zahera amtolea uvivu Lwandamina kisa kaifundisha Yanga, awataja Simba ‘Ilikuwa Yanga yazamani sio hii, awalete tu Zesco

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema haofii chochote kuelekea kwenye mchezo wao wa mzunguko wa kwanza wa  klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Zesco United kutoka Zambia.
Image result for Mwinyi Zahera
Zahera ameyasema hayo kupitia kipindi cha Yanga Tv kilichorushwa na Azam Tv hapo jana saa 1 : 00 usiku na kuongeza kitendo cha Georg Lwandamina kuwahi kuifundisha Yanga SC hakimnyimi usingizi kuelekea mechi hiyo.
Zahera amtolea uvivu Lwandamina kisa kasikia kafundisha Yanga, aitaja Simba ”Ya leo sio ya kesho na ya kesho sio ya leo, Ailete tu Zesco
”Kocha yule kuwa amepita Yanga SC, ile ilikuwa yazamani hata wachezaji wengi aliyowahacha hawapo tena. Mpira una mambo mengi ya leo sio ya kesho na ya kesho sio ya leo.
”Alipita Yanga, alishapita hapa sasa ni Zesco dhidi ya Yanga ndiyo watacheza, sisi tunamipango yetu na wao wanampango yao.
Zambia nchi ambayo inatoka klabu ya Zesco United inashika nafas ya 81 katika ubora wa viwango vya soka duniani wakati Tanzania inapotokea Yanga SC ipo kwenye nafasi ya 137.
Katika hilo Zahera amesema haitoshi kuwa sababu ya timu yake kuihofia Zesco ”Mpira wa Congo, Misri na Algeria ni mkubwa kushinda wa Tanzania ?, Simba aliwapiga hapa wa Misri, alimpiga Vita Club na aliipiga timu ya Algeria hapa na mpira wao mkubwa kuliko wa Tanzania, sasa sijajua namna gani Yanga asimpige Zesco.”
”Hatakama Zambia ina ligi bora sisi hatuwezi kuogopa timu kama Zesco, hatuwezi tunacheza mpira tukiwa na lengo moja na inawezekana.”
Yanga inaweka kambi jijini Mwanza ambapo itacheza mechi mbili za kirafiki ambazo ni  Mbao FC na Pamba Sports Club ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na mkondo wa kwanza wa mzunguko wa kwanza ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United kutoka Zambia itakayochezwa siku ya Jumamosi tarehe 14 ya mwezi ujao.

"Akili ndogo kujadili mambo makubwa'' - Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda, amewashangaa watu wanaohoji kitendo cha Rais Magufuli kukutana na watendaji wa kata, ambapo amesema kuwa wengi ambao wamekuwa wakihoji walishashindwa kutimiza majukumu yao kwa wananchi.

Makonda ameyabainisha hayo leo Agosti 31, 2019 wakati akizungumzia ujio wa ugeni ikiwa ni pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa kuona umuhimu wa kukutana na viongozi hao wa ngazi ya chini.
“Dkt Magufuli alichokiamua hata akitaka kukutana na wenyeviti wa mitaa na penyewe mtasema wote anataka wahamie CCM, unajua shida moja tunaruhusu akili ndogo kujadili mambo makubwa, na sisi watanzania wengi tunapoteza sana muda kufikiria vitu kwa njia hasi'', amesema Makonda.
Aidha Makonda amewataka watendaji hao wanaokuja jijini humo kutokuwa na hofu ya kuibiwa mali zao, kwani jiji hilo kwa sasa halina wizi wa namna hiyo kama ambavyo watu wa mikoa mingine wamekuwa wakifikiria.
Rais Magufuli atakutana na watendaji wa Kata nchi nzima Ikulu ya Dar es Salaam siku ya Septemba 2, 2019.

Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumamosi

Mwenyekiti wa Crystal Palace Steve Parish amesema atamruhusu mshambuliaji wa Ivory Coast forward Wilfried Zaha, 26, kuondoka klabu hiyo msimu ujao wa uhamisho wa wachezaji- ikiwa dau lililotangazwa na Arsenal na Everton litafikiwa. (Daily Mail)
Parma wamekubali mpango wa kumsajili beki wa Manchester United Matteo Darmian kw euro milioni 1.4 (Sky Sports)
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amekasirishwa na hatua ya viongozi wakuu wa klabu hiyo kushindwa kumsajili Paul Pogba,26, kutoka Manchester United. (Sports)
Neymar ameifahamisha Paris St- Germain kuwa yuko tayari kurudi chini na kuboresha uhusiano wao endapo atakosa nafasi ya kuhamia Barcelona ama Real Madrid kabla dirisha la uhamisho wa wachezaji Ulaya kufungwa msimu huu.( Independent)

NeymarHaki miliki ya pichaAFP
Image captionNeymar, nyota wa soka wa kimataifa wa Brazil

Huku hayo yakijiri, mkurugenzi wa kiufundi wa Paris St-Germain Leonardo amesema mabingwa hao wa Ufaransa hawajakaribia kufikia makubaliano na Barcelona kumhusu Neymar. (Marca)
Meneja wa klabu ya Barcelona Ernesto Valverde amesema kuwa amechoshwa na mashauriano yanayozunguka uhamisho wa Neymar kuja klabu hiyo (Standard)
Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amesema kuwa mlango upo wazi kwa kiungo wa kati wa klabu hiyo Mesut Ozil kurejesha hadhi ya mchezaji nyota wa Gunners.(Mirror)

Mesut Ozil
Image captionMesut Ozil, Kiungo wa kati wa Arsenal

Paris St-Germain wamewatambua wachezaji kiungo wa kati wa Tottenham Christian Ericksen 27, na mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala,35,kama wachezaji wawil8 watakao chukua nasi ya Neyma endapo atahamia Barcelona (Le Parisien kwa kifaransa)
Atletic Madrid wanatafakari uwezekano wa kusajili kwa mkopo mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icadi na baadae kumnunua kwa euro milioni 70 (ESPN)
Real Madrid imekubali kuiuzia Paris St-Germain kipa wake Keylon Navas,32, ikiwa klabu hiyo itakubali kumuachilia Alphonse Riola kujiunga nao kwa mkopo (Star)
Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Fernando Llorente,34, amekubalia kutia saini mkataba wa miaka miwili na Napoli inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia, Serie A (Sky Sports)
Kiungo wa Kati wa Sportings Bruno Fernandes aliyehusishwa na tetesi za uhamisho kwenda Manchester United na Tottenham msimu wa joto hatimae ametua Real Madrid baada ya kutiavsaini mkataba wa euro milioni 63 (Mail)

Waziri Ummy atoa tahadhari ya Ebola kwa wananchi

Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu ametoa tahadhari ya Ugonjwa wa Ebola kwa Wananchi katika mikoa yote ya Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya, imetoa elimu kwa watanzania juu ya namna ya kuepuka ugonjwa huo ambao ni hatari.
Waziri Ummy amewataka wananchi kuchukua hatua stahiki za kujikinga na kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini.
Ebola imekuwa tishio kwa nchi kadhaa zinazopakana na Tanzania ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Tazama Video hapo chini ikieleza namna ya kujinga au kujua dalili za Ebola.

Wizara inapenda kutoa Tahadhari ya Ugonjwa wa Ebola kwa Wananchi katika Mikoa yote ya Tanzania na pia kuwataka kuchukua hatua stahiki za kujikinga, na kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini mwetu@Waziri Ummy Mwalimu@umwalimu@DocFaustine

36 people are talking about this

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list