Kuelekea ya Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya pili dhidi ya Zesco, Mkurugenzi mpya wa ufundi wa klabu ya Yanga ambaye atatokea nchini Uingereza, anatarajia kuanza kazi rasmi leo.
Mkurugenzi huyo, aliyekuwa anafanya shughuli za soka nchini Uingereza ni Mtanzania, aliyezaliwa visiwani Zanzibar akiwa amebobea katika masuala ya ufundi na program za vijana.
Mmoja wa viongozi wa Kamati ya Utendaji wa Yanga alisema tofauti na ufundi, wakurugenzi wengine watakaonza kazi leo ni wa Masoko, Fedha na Sheria.
Kiongozi huyo alisema hawajaweka majina ya watu hao hadharani kutokana na kuwa walikuwa bado katika ajira na waliakubaliana leo ndiyo wanaweza kuwaweka wazi wakati wanapoanza majukumu yao rasmi.
“Rasmi kesho (leo), Mkurugenzi wa Ufundi ataanza kazi, anatokea Uingereza lakini ni Mtanzania aliyezaliwa Zanzibar, mkurugenzi wa masoko, sheria na fedha.
Kamati ya Utendaji ya Yanga, inatarajia kukutana leo na hao waajiriwa, baada ya hapo majina na CV zao zitawekwa wazi, tulishindwa kufanya hivyo mapema kwa kuwa walikuwa bado katika ajira,” kilisema chanzo.
Alieleza kuwa nafasi nyingine ikiwamo ya katibu, ofisa mtendaji mkuu na ofisa habari, zinaendelea kushughulikiwa na kamati husika
No comments:
Post a Comment