Kiungo mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib ameeleza kutofurahishwa na baadhi ya mashabiki wa Yanga ambao wamekuwa wakimzungumza vibaya licha ya kuifanyia mema klabu hiyo misimu miwili aliyoitumikia
Ajib alirejea Simba msimu huu baada ya kumaliza mkataba Yanga. Kuondoka kwake Yanga kumewavuruga baadhi ya mashabiki wa timu hiyo aliyokuwa nahodha na mmoja wa watia saini wa akaunti iliyokuwa imeanzishwa kuichangia timu hiyo
Ajib amesema baadhi ya maneno ya mashabiki yanamfanya ajitume zaidi lakini wengine wanamkosea heshima licha ya mema aliyoifanyia Yanga
"Najua ni maneno ya mashabiki ambayo siku zote hawataki kukubaliana na hali ilivyo, lakini nashangaa kuona wananizungumzia kwa mabaya tu, wakati yapo mazuri niliyofanya," amesema
“Muda mwingine maneno yao yananipa nguvu ya kujituma mazoezini ili niweze kuipa matokeo bora Simba na kuwanyamazisha, lakini nakereka na kuumia sana na maneno yao wanayonizungumzia wakati niliishi nao vizuri”
"Mchezaji kutoka sehemu moja kwenda nyingine si kosa na kumzungumzia vibaya au kumhusisha na mambo ya kichonganishi si vizuri kwa sababu ipo siku naweza kurudi Yanga, jambo zuri ni kukubaliana na uhalisia ulivyo"
No comments:
Post a Comment