Nahodha msaidizi wa Yanga Mrisho Ngasa amesema wanajiandaa kikamilifu kushinda mchezo wa nyumbani wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United ambao utapigwa Septemba 14 kwenye uwanja wa Taifa
Ngasa amesema hesabu zao ni kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa
Kwenye mchezo wa nyumbani hatua ya awali dhidi ya Township Rollers, Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 hivyo kulazimika kushinda ugenini na hatimaye kufanikiwa kutinga raundi ya kwanza
"Tunaanzia nyumbani, hatupaswi kufanya makosa kama ilivyokuwa mchezo dhidi ya Rollers, tunahitaji ushindi," amesema
"Ushindi wa nyumbani utatupungizia presha ya mchezo wa ugenini hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi"
"Tumejiwekea malengo ya kuingia hatua ya makundi. Lolote linaweza kutokea tukishaingia hatua hiyo"
No comments:
Post a Comment