Beki wa kulia wa Simba Zana Coulibaly amerejea nchini kuongeza mkataba kunako klabu ya Simba
Inaelezwa beki huyo raia wa Burkina Faso atasaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabingwa wa nchi
Kumekuwa na maoni tofauti miongoni mwa wadau wa klabu ya Simba kuhusu kuongezwa mkataba kwa beki huyo
Hata hivyo kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ameonyesha kuwa na imani nae
Mara nyingi amesisitiza kuwa Zana ni mchezaji mzuri, anachohitaji ni muda ili kuweza kudhihirisha ubora wake
Mchakato huo wa kumuongezea Zana mkataba ukikamilika, Simba itakuwa imebaki na nafasi moja ya mchezaji wa kigeni ambapo nafasi hiyo huenda ikachukuliwa na kiungo Francis Kahata hivyo kuachana rasmi na Emmanuel Okwi na Walter Bwalya

No comments:
Post a Comment