Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema katika kipindi cha siku mbili watampokea mshambuliaji mpya ambaye amesajiliwa kuongeza nguvu kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa
Baada ya kutua mkoani Morogoro juzi, jana Zaheara ameanza majukumu yake katika benchi la ufundi
Mcongomani huyo amesema kikosi chake kimeimarika kiasi lakini bado kinahitaji marekebisho
"Nimewaona vijana wangu, wameimarika kiasi fulani lakini sio sana bado kuna marekebisho," amesema
"kikosi kilichocheza jana sio kilichocheza juzi , wale waliocheza juzi watacheza kesho asubuhi tutakuwa na mchezo mwingine wa kirafiki
"Malengo yangu kuhusu usajili yametimia ila bado striker mmoja ambaye atawasili kesho ama keshokutwa akishafika mambo yatakuwa yamekamilika na ntaiandaa timu kamili kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa"
Leo Yanga itacheza dhidi ya Friends Rangers kutoka jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment