Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amemaliza sintofahamu iliyokuwa ikiwakabili walinzi Juma Abdul na Andrew Vicent Chikupe ambao hawakuingia kambini mkoani Morogoro kutokana na kuwa na madai kwa uongozi wa klabu hiyo
Zahera amesema kuwa alizungumza na wachezaji hao ambapo walimueleza matatizo yao na wamekubaliana, watarejea kujiunga na wenzao baada ya changamoto zinazowakabili kupatiwa ufumbuzi
Amesema uongozi wa Yanga unashughulikia madai yao na suala hilo litamalizika ndani ya muda mfupi
Wachezaji hao walishindwa kuingia kambini mkoani Morogoro wakisubiri kupatiwa ufumbuzi wa madai yao
Juzi akiwa visiwani Zanzibar, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alisema suala la wachezaji hao walilikabidhi kwa kocha Zahera
No comments:
Post a Comment