Habari njema kwa Wanayanga ni kuwa kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera amewasili Alfajiri ya leo na ataelekea moja kwa moja mkoani Morogoro
Kulingana na taarifa aliyoitoa juzi, Zahera alipewa mapumziko ya siku 15 baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa kwenye michuano ya Afcon 2019 na anapaswa kuwa amerejea kazini ifikapo Julai 28
Zahera atakuwa na wiki moja ya kukinoa kikosi chake kabla ya mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi August 04 dhidi ya Kariobangi Sharks na wiki mbili kuelekea mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers
Juzi Mcongomani huyo aliwashukia waandishi wa habari waliozusha kuwa amegoma kurudi nchini kwa kuwa anaidai Yanga
"Siidai Yanga hata elfu moja, sikuwahi kutoa fedha za usafiri wala kulipia gharama za kambi, yote wanayosema ni uongo.."

No comments:
Post a Comment