We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 8, 2019

YANGA YATIMKIA MOROGORO

Leo kikosi cha Yanga kinaelekea mkoani Morogoro kuanza maandalizi ya msimu mpya
Yanga inakwenda Morogoro ikiwa na nyota wake wote ambao hawakuwa na majukumu ya timu za Taifa kwenye michuano ya Afcon 
Wachezaji walioshiriki Afcon wamepewa mapumziko ya siku 10
Yanga inaanza maandalizi chini ya kocha msaidizi Noel Mwandila wakati kocha Mwinyi Zahera atajiunga na timu baada ya siku 10
Zahera alishatuma programu yote ya mazoezi ambayo itasimamia na Mwandila wakati ambao yeye hatakuwepo
Baada ya kukosa ubingwa wa ligi kuu kwa misimu miwili mfululizo,  lengo la kwanza msimu ujao ni kurudisha ubingwa Jangwani
Lakini pia Yanga inarejea kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kukosa kwa msimu mmoja
Wakati Simba wakitamba kwa kufanikiwa kutinga robo fainali msimu uliopita,  Yanga ina mtihani wa kuhakikisha inafanya vizuri kwenye michuano hiyo
Mabingwa hao wa kihistoria watahitaji angalau kufika hatua ya makundi
Usajili uliofanywa ni wa uhakika na jambo jema ni kuwa wachezaji wote waliosajiliwa walipendekezwa na Zahera isipokuwa mchezaji mmoja tu aliyesajiliwa juzi kuchukua nafasi ya Gadiel
Hata hivyo Zahera aliupa baraka zote uongozi wa Yanga kuziba nafasi ya Gadiel
Wana Jangwani wanasubiri kuiona timu yao, bila shaka Julai 27 wataishuhudia kwa mara ya kwanza uwanja wa Taifa, kilele cha siku ya Mwananchi
Siku hiyo watawafahamu wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao ambapo Yanga itashuka dimba la Taifa kucheza mchezo wa Kimataifa wa kirafiki

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list