Mshambuliaji wa FC Renaissance David Molinga Ndama ndiye aliyetua usiku wa kuamkia leo kukamilisha dili la kujiunga na Yanga
Alijiunga na FC Renaissance akitokea klabu ya Fc Lupopo ambayo pia alicheza Heritier Makambo
Molinga ni jembe hasa la kazi, msimu uliopita alikuwa kinara wa upachikaji mabao hapo FC Renaissance
Aliifungia timu hiyo mabao 11 akishika nafasi ya tano vinara wa kupachika mabao ligi kuu ya Congo ambayo mfungaji bora Jackson Muleka wa TP Mazembe alifunga mabao 16
Ujio wake umefanikishwa na kocha Mwinyi Zahera na anatajwa kuchukua nafasi ya Mcongo mwenzie Klaus Kindoki
Ni pande la miraba minne, walinzi njaa njaa watakuwa na kazi kubwa ya kumzuia mtu huyu
No comments:
Post a Comment