We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, July 11, 2019

Yanga yaahirisha tamasha la Siku ya Mwananchi


Uongozi wa klabu ya Yanga umesogeza mbele tamasha la Siku ya Mwananchi hadi hapo watakapotangaza tena ili kupisha maandalizi ya mechi Taifa Stars ya kusaka kufuzu kwa CHAN2020.

Tanzania itacheza na Kenya kati ya Julai 26 na Julai 28 katika mchezo wa kwanza wa kusaka kufuzu kwa fainali hizo za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani.
Tamasha hilo lenye lengo la kutambulisha wachezaji pamoja kufanya shughuli za kijamii lilipangwa kufanyika Julai 28 mwaka huu sasa limesogezwa mbele hadi hapo tarehe nyingine.
Akizungumza Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Dismas Ten alisema sababu za kusogezwa kwa tamasha hilo ni kupisha mashindano ya CHAN.
Alisema maandalizi kuelekea tamasha hilo yataendelea kama kawaida hadi hapo tamasha hilo litakapopangiwa tarehe.
"Kikosi kitaendelea na maandalizi Morogoro kambini hadi kamati ya maandalizi ya tamasha hilo itakapotangaza tarehe," alisema Tena.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list