We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, July 28, 2019

YANGA WABIDHI MSAADA HOSPITALI YA MWANANYAMALA

YANGA Tawi la nguvu ya Buku lenye makazi yake Mwananyamala leo wamekabidhi rasmi msaada wa ukarabati wa Wodi ya Wanaume no.5 waliokuwa wakifanya kwa takribani wiki moja kuelekea kilele cha siku ya Wananchi inatarajiwa kuadhimishwa na Klabu ya Yanga Jumapili ya Agosti 4,2019.

Akizungumza na Wanahabari mara baada ya makabidhiano Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Mussa Wambura aliwapongeza Wanayanga tawi la Nguvu ya Buku kwa fikra za msaada walioufikiria na fundisho tosha kwa wengine.
Alisema Wambura, msaada wa kitendo mlichokifanya kitabaki kuwa Historia kwa Hospitali ya Mwanabyamala na kuwaomba jamii ziige kutoa misaada ya namna hii inayomgusa kila binadamu kwani Hospitali ni yetu sote tusiiachie Serikali tu, jukumu hili ni la kila mmoja.Leo mmefanya Tawi la Nguvu ya Buku tunaomba wajitokeze na wengine.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Sindano Mwananyamala ambako Tawi hilo linapatikana aliwapongeza sana Tawi la Nguvu ya Buku kwa kitendo cha Kijamii walichokifanya na hakika yeye kama mpezi wa upande wa pili wamejifunza kitu ambacho kinastahili kuigwa na Mwananchi yeyote anayejitambua.

Nae Mwenyekiti wa Nguvu ya Buku, Ally Kuacha aliwapongeza wanachama wake kwa kujitoa mpaka kukamilisha mchakato mzima waliokuwa wamekusudia kuelekea kilele cha siku ya Wananchi na kuwaomba waendelee na mshikamano huohuo siku zote.
Mwisho Katibu wa Tawi la Yanga la Nguvu ya Buku, Juma Iyagala alisema ukarabati huo wa Wodi ya Wanaume umegharimu Shilingi 1,830,000/= ambao ni kupaka rangi ndani na nje, kupaka rangi bati pamoja na kubadilisha nyavu za mbu.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list