Baada ya maandalizi ya wiki tatu mkoani Morogoro, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam Ijumaa August 02 2019 siku mbili kabla ya siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi
Yanga itakuwa tayari kwa tukio hilo la kihistoria litakalofanyika Jumapili ya August 04, uwanja wa Taifa
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera aliyewasili mkoani Morogoro jana, atakuwa na takribani siku tano kukinoa kikosi chake kabla ya kuivaa Kariobangi Sharks Jumapili
Mcongomani huyo amesema amefurahishwa na maandalizi yaliyofanywa kocha Msaidizi Noel Mwandila wakati ambao yeye hakuwepo
Amesema atatumia muda uliobaki kuwaandaa wachezaji wake kimbinu tayari kwa mchezo wa Jumapili na mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers
Yanga ikiwa chini ya Noel Mwandila, imecheza michezo mitano ya kirafiki na kufanikiwa kushinda yote

No comments:
Post a Comment