Yanga huenda ikasajiliwa wachezaji wawili kabla ya dirisha la usajili wa ndani kufungwa Julai 31
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten ambaye ndiye msemaji wa klabu hiyo, amefichua mpango huo
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Ten ameandika;
"Usajili wa ndani unafungwa tarehe 31/July bado tuna nafasi mbili.....!Ndo tunarudi hivyo kusinya Tukutane Taifa tarehe 4, Mwaka huu wasipoweka mpira kwapani hehehe.."
Dirisha la usajili Tanzania linatarajiwa kufungwa Julai 31
Yanga inahusishwa kuwa kwenye mpango wa kumsajili beki Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union
Mabeki Andrew Vicent Chikupe na Juma Abdul waligoma kuingia kambini mkoani Morogoro wakishinikiza walipwe madai ya fedha za usajili
Huenda mpango huo ukawahusu wachezaji hao

No comments:
Post a Comment