We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, July 7, 2019

Wazee ACT-Wazalendo walia matukio ya utekaji nchini Tanzania


By Fortune Francis, Mwananchi ffrancis@mwananchi.co.tz

Ngome ya wazee ya chama cha ACT- Wazalendo imeitaka Serikali ya Tanzania kukomesha matukio ya utekaji yanayoripotiwa maeneo mbalimbali nchini.
Hayo yameelezwa leo Jumapili Julai 7, 2019 na mwenyekiti wa ngome hiyo, Wilson Mushumbusi wakati akitoa maazimio ya kamati ya uongozi.
"Serikali ichukue hatua kuhakikisha inakomesha vitendo vya watu kutekwa na wale wanaojiita wasiojulikana, lakini pia waliotekwa waachiwe huru.”
"Haileti maana mtu anatekwa mchana kweupe au mbele za watu lakini watekaji hawapatikani, wakati mwingine watekaji  wanakuwa na silaha,” amesema Mushumbusi.
Katika kikao hicho cha siku moja kamati hiyo ilijadili mambo mbalimbali ya kisiasa, kijamii na uchumi na kuweka mipango kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Oktoba 2019, na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list