Amedai mwanamke huyo aliwachukua wasichana kutoka Tanzania Bara kufanya kazi kwenye baa iliyopo Zanzibar, badala yake alikuwa akiwatumikisha kingono.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Julai 7, 2019 amesema amechukua uamuzi huo kwa kuwa kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo ni kinyume na sheria za nchi, kubainisha kuwa kwa sasa mwanamke huyo anashikiliwa na kutoweka wazi mahali alipo.
Amebainisha kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) haipo tayari kuona wananchi wanateseka kwa ajili ya maslahi ya watu wachache, huku wakifanyishwa shughuli kinyume na matakwa yao.
Amesema mwanamke huyo alikuwa akiishi Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja ameshahojiwa na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto.
“Kama kuna haki anazodaiwa na wasichana aliowachukua huko Tanzania Bara aweze kuwalipa kwa mujibu wa sheria za kazi,” amesema.

No comments:
Post a Comment