Na Timothy Itembe, Mara
Mbunge wa viti maalumu Tanzania kupitia Chama cha mapinduzi CCM,Amina Makilagi amewataka wanachama wa Chama cha mapinduzi CCM kumuunga mkono Rais awamu ya Tano,DT John Pombe Magufuli katika juhudi za kutekeleza shuguli za maendeleo kwa jamii.
"Shuguli za maendeleo kwa jamii anazotekeleza Rais John Pombe Magufuli wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuna haja ya kumuunga mkono kwasababu lengo ni Taifa letu kuondokana na umasikini,Ujinga huku tukipambana na maradhi na kwa kuwa mimi ni Mbunge ambaye ninatokana na CCM Mmi ni wa kwanza kumuunga mkono Rais wetu kulingana na katiba yetu"alisema Makilagi.
Makilagi aliongezsa kuwa Rais Magufuli na viongozi wengine waliotangulia kabla yake wamefanya kazi kubwa ya kujenga Taifa la Tanzania ili kuhakikisha kwamba Wananchi wake wanapata hudumas mhimu za kijamii huku wakinufaika na matunda ya Uhuru wao.
Pia Mbunge huyo aliongeza kuwa Rais Magufuli ametekeleza miradi mikubwa ndani ya Tanzania na amejenga imani kwa Watanzania pamoja na Mataifa mengine anasifika kuwa kiongozi Bora.
Makilagi alitumia nafasi hiyo kuchangia Ofisi ya Jumuia ya Wanawake Tanzania UWT Wilaya Tarime Kumpyuta mashine ikiwa na vifaa vyake kwa lengo la kuchapisha machapisho pamoja na kuandalia taarifa mbalimbali za kiofisi Ofisini kwao na kuondokana na kero ya kwenda kuandaa taarifa za Jumuia ya UWT kwenye vibanda vya watu binafsi ambavyo sio sehemu salama.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha mapinduzi wilayani Tarime mkoani Mara,Khamisi Mkaruka alisema kuwa licha ya kuwa wilaya Tarime kwa maana ya majimbo yake mawili Tarime Vijijin inayoongozwa na John Heche na Tarime Mjini iliyo chini ya Esther Matiko chini ya Upinzani kwa maana ya Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema wanaimani kuwa majimbo hayo kwa uchaguzi ujao yanaenda kurudi ndani ya CCM.
Mkaruka aliongeza kuwa kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa Chama chake kimejipanga kuhakikisha kuwa Chama hicho kinaenda kupata viti vingi tofauti na uchaguzi wa mwaka uliopita ambapo upinzani kwa maana ya Chadema walikuwa na viti vingi hata kuongoza halmashauri kwa maana ya madiwani wake kuwa wengi.

No comments:
Post a Comment