We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, July 9, 2019

Wakili akwamisha kesi ya Halima Mdee



By Fortune Francis, Mwananchi ffrancis@mwananchi.co.tz

Kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Tanzania, John Magufuli inayomkabili mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee imekwama kuendelea leo Jumanne Julai 9, 2019 katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kutokana na wakili anayeiendesha kuwa mgonjwa.
Wakili wa Serikali, Glory Mwenda amedai leo mbele ya  hakimu mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini wakili, Patrick Mwita anayeiendesha ni mgonjwa.
Kufuatia maelezo hayo, hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 30, 2019 na kuutaka upande wa mashtaka kuleta mashahidi waliobaki ili kesi hiyo imalizike kwa wakati kwa kuwa ni ya muda mrefu.
Hadi sasa mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi akiwemo mkuu wa kituo cha polisi cha Urafiki, mrakibu wa Polisi (SP), Batseba Kasanga.
Katika kesi ya msingi inadaiwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya  Rais Magufuli kuwa,  “anaongea hovyo, anatakiwa  afungwe breki”,  kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani.



No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list