We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, July 3, 2019

Ushahidi wa mauaji, washindwa kuteketezwa

Uteketezwaji wa vielelezo vilivyotumika katika kesi ya mauaji, ya mwanafunzi wa shule ya Scolastica Humphrey Makundi,  umeshindwa kuteketezwa leo Julai 3, baada ya wateja upande wa mawakili watetezi kutokuwepo Mahakamani hapo.

Akiwasilisha ombi la kusitisha kazi hiyo, mbele ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi, wakili Elikunda Kipoko amebainisha umuhimu wa wateja wake kuwepo, ukizingatia baadhi yao wameshakata rufaa.
Ikumbukwe kuwa wakati hukumu  ya kesi hiyo ikitolewa siku ya Juni 3, 2019, Jaji wa Mahakama Kuu Firmin Matogolo, aliagiza vielelezo likiwemo panga lililotumika katika mauaji, na nguo za marehemu kuteketezwa, na kuagiza vielelezo vingine kama vile simu,  iliyotumika kuwasiliana usiku na kuitana eneo la tukio, Jaji aliamuru vitaifishwe na Serikali.
Juni 3, 2019 Mahakama hiyo ilimhukumu kunyongwa hadi kufa, aliyekuwa mlinzi wa shule hiyo, Hamis Chacha, huku mmiliki wa shule hiyo Edward Shayo pamoja na aliyekuwa mwalimu wa nidhamu, Laban Nabiswa wakihukumiwa kifungo cha miaka minne jela, kwa kuficha ukweli wa mauaji ya mwanafunzi huyo.
Aidha Naibu msajili wa Mahakama hiyo, Frank Mahimbari, amesema kutokana na kuwa washtakiwa wote hawapo mahakamani, hivyo ataandika samansi ili waletwe mahakamani kushuhudia zoezi hilo.
Humphrey Makundi(16) aliuawa Novemba 6, 2017, na kisha mwili wake kutupwa katika mto Ghona, takribani mita zaidi ya 250 kutoka eneo la shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list