We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 8, 2019

Tshishimbi abariki Gadiel kuondoka Yanga



Baada ya taarifa za beki wa Yanga, Gadiel Michael kuhusishwa kutua Simba, kiungo Papy Tshishimbi ameibuka na kusema kuondoka kwake siyo tatizo kwa miamba hiyo ya mtaa wa Jangwani na Twiga.

Gadiel alikuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza cha Yanga kilichomaliza ligi katika nafasi ya pili msimu uliopita amemaliza mkataba na Wanajangwani na taarifa za ndani zimebainisha kuwa tayari amemwaga wino Msimbazi.
Tshishimbi alisema Gadiel alikuwa na umuhimu kikosini alipokuwepo, lakini mara baada ya kuondoka umuhimu wake unakuwa haupo na wachezaji wengine watafanya majukumu hayo.
"Yanga ina wachezaji wengi na mchezaji kuhama katika klabu moja kwenda nyingine hilo suala lipo wala halijaanza leo hivyo kwakuwa kaondoka mapema usajili ukiwa bado unaendelea naamini viongozi watafanyia kazi hilo,"
"Hakuna mchezaji muhimu zaidi kwenye klabu ambayo inasajili anaweza akaondoka na akasajiliwa mwingine bora zaidi na mchezaji huyo ambaye wengi waliona ni pengo hakawa hakumbuki hata kwa sekunde," alisema.


Tshishimbi ni rafiki wa karibu na mchezaji huyo alisema hawezi kuzungumzia nafasi ya mchezaji huyo katika kikosi chake kipya kwa sababu hana uzoefu na timu nyingine.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list