We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, July 25, 2019

TFF: Tumepata mdhamini wa Ligi Kuu Bara

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema tayari wamepata mdhamini wa Ligi Kuu Bara msimu ujao atatangazwa hivi karibuni.
Karia amesema mchakato wa mdhamini umefanywa siri kwa sababu maalumu, ingawa amesisitiza hadi Agosti 15 watamtangaza mdhamini huyo na wameingia naye mkataba wa miaka mingapi.
"Kila kitu kinakwenda vizuri kuhusu mdhamini na kabla Ligi haijaanza tutamuweka wazi," alisema Karia mbele ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.
Karia alisema awali walishindwana na baadhi ya wadhamini waliokuwa wamejitokeza kwa kuwa TFF haikutaka kujishusha na kufuata masharti ambayo mdhamini aliyataka.
"Mdhamini anapaswa kuona thamani ya Ligi, lakini si kutushusha na kutaka tufuate vile atakavyo, lakini sasa tumeshapata mdhamini na kila kitu kinakwenda sawa," alisisitiza.
Wachezaji wa Kigeni ruksa ila kwa mashartiAlizishauri klabu za Ligi kutafuta pia wadhamini wake ambao ndiyo wana mamlaka ya kukaa kwenye jezi ya timu na wale wa TFF wanawekwa mabegani.
Katika hatua nyingine waziri Mwakyembe alisema wamekutana na viongozi wa TFF na kuweka msimamo kwa wachezaji watakaosajiliwa kuchezea klabu za Soka nchini.
"Mwanzo tulipata wakati mgumu kuridhia utaratibu wa wachezaji 10 wa kigeni kusajiliwa katika kila klabu, lakini tumezungumza na TFF juu ya faida za wachezaji wa kigeni kwenye Ligi zetu," alisema.
Alisema wameridhia idadi hiyo ya wachezaji 10 iendelee, lakini kwa sharti kwamba wale watakaosajilia sharti wawe wanachezea timu zao za Taifa kwenye nchi wanazotoka.
"Pia wawe wanatokea kwenye klabu zinazoshiriki Ligi Kuu huko walikotoka," amesisitiza Mwakyembe katika mkutano wake na viongozi wa TFF.
Karia alisema mkakati huo utafanyiwa kazi ingawa kuna baadhi ya nchi ambazo soka lao liko juu kulinganisha na Tanzania, hivyo ikitokea wachezaji wa Ligi daraja la pili au la kwanza kutoka kwenye hizo nchi nao watakuwa huru kusajiliwa.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list