We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, July 25, 2019

Bodi ya Ligi: Hatukujua Simba itaanzia hatua za awali kimataifa

Bodi ya Ligi Tanzania (TPBL) imesema haikujua kama timu ya Simba itapangwa kucheza hatua za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika ndiyo sababu waliipanga kucheza mechi za ufunguzi wa Ligi Kuu.
Ratiba ya Ligi inaonyesha Simba itacheza na JKT Tanzania Agosti 23 mchezo wake wa kwanza huku ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ikionyesha timu hiyo itacheza mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya UD Songo ugenini kati ya Agosti 23-25.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema, wakati wa kupanga ratiba ya Ligi Kuu hawakutarajia kama Simba ingeanzia hatua ya awali kwenye Ligi ya Mabingwa ndiyo sababu waliwapangia kucheza mechi za ufunguzi za Ligi Kuu.
"Kwa kuwa Simba ilitolewa katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, tulitegemea wakianza mashinmdano ya CAF msimu ujao hawataanzia hatua za awali na imekuwa tofauti," alisema.
Alibainisha kwamba, kutokana na ratiba hiyo, watakaa na Simba na kuweka mambo sawa ili kuona ni namna gani watacheza mechi hiyo ya ufunguzi wa Ligi.
Awali, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alieleza namna alivyochukizwa na viporo vya Ligi ya msimu uliokwisha.
 "Kwa namna viporo vilivyokuwa vingi, Ligi yetu ingeingia hata kwenye kitabu cha maajabu ya dunia, tumelijadiri hilo na TFF na Bodi ya Ligi ambao wamenihakikishia kuwa hilo halitojirudia," alisema Dk Mwakyembe.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list