Katika kutekeleza adhma ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Tanzania (TFDA) ambayo kwa sasa inajulikana kama Tanzania Medicines and Medical Devices Authority (TMDA), imefuta tozo 9 na kuhamisha majukumu ya udhibiti wa chakula na vipodozi kwenda TBS.
Pia Naibu waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile amesema TFDA sasa kusimamia dawa na vifaa tiba pekee, majukumu yake ya awali yamehamishiwa TBS.
“Kuanzia tarehe 1 Julai, 2019 Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA itajulikana kama kama Tanzania Medicines and Medical Devices Authority (TMDA). Taasisi hii itasimamia masuala ya dawa na vifaa tiba pekee. Majukumu udhibiti ya chakula na vipodozi yatafanywa na TBS,” amesema Naibu waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile.

No comments:
Post a Comment