Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema hana uhakika kama Neymar, 27, atakuwa na makali yaleyale aliyokuwa nayo kabla atakaporejea klabu ya Barcelona akitokea klabu ya Paris St-Germain. (Ara, via Mirror)
Manchester United wameshaafikiana kuhusu matakwa binafsi na mshambuliaji wa Sevilla Wissam Ben Yedder, 28. Mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa anatarajiwa kujiunga na mashetani hao Wekundu endapo mshambuliaji wa Ubelgiji Romelo Lukaku atauzwa ama la. (Express)
Manchester United wanaweza kuwapoka Tottenham tonge mdomoni katika usajili wa kiungo wa klabu ya Lyon ya Ufaransa, Tanguy Ndombele. Spurs tayari wameshakubali kumnunua mchezaji huyo lakini hawajamalizana naye kuhusu matakwa yake binafsi mchezaji huyo mwenye miaka 22. (L'Equipe, via Metro)
Liverpool wanaweza kumrudisha kiungo mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 27, baada ya mchezaji huyo kushindwwa kuwa na wakati mzuri kwenye klabu ya . (Le10 Sport, via Mirror)
Kiungo wa Aston Villa John McGinn anaweza akatakiwa na Manchester United, ambao itawabidi walipe kitita cha pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uskochi. (Sun)
Real Madrid wanataka kuwapa Liverpool kiungo Mhispania Marco Asensio, 23, lakini wanataka mshambuliaji machachari wa Senegal Sadio Mane, 27, awe sehemu ya mabadilishano hayo. (Express)
Tottenham wanatarajiwa kumpeleka kwa mkopo kiungo wake kinda Jack Clarke 18, katika klabu yake ya zamani ya Leeds United. (Guardian)
Derby County wanapanga kumsajili mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi Phillip Cocu kama kocha atakayerithi mikoba ya Frank Lampard ambaye anatarajiwa kujiunga na klabu ya Chelsea muda wowote ule. (Times - subscription required)
Leeds wanataka kumsajili mshambuliaji wa Ecuador Felipe Caicedo, ambaye anachezea klabu ya Lazio ya Italia na ameshawahi kuchezea klabu ya Manchester City. (Imperio, via Star)
Klabu ya Juventus inapanga kumsajili winga wa kinda wa Burnley na England, Dwight McNeil, 19. (Sun)
Juventus pia inataraji kuwauza viungo wake wawili Blaise Matuidi na Sami Khedira wote wenye miaka 32. (Tuttosport, via Calciomercato)
No comments:
Post a Comment