Licha ya kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba Yanga, beki wa kushoto Gadiel Michael bado hajasaini, akitaka apewe muda zaidi
Aidha kuna taarifa kuwa Gadiel ametaka kuongezewa dau la usajili
Ikumbukwe Gadiel alifanya majaribio kunako klabu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini mwezi April, inadaiwa anasikilizia ofa ya timu hiyo
Mabosi wa Kamati ya usajili ya Yanga chini ya Mwenyekiti Frank Kamugisha wako Misri kukamilisha usajili wa nyota wanaoshiriki michuano ya Afcon
Wamefanikiwa kuwapa mikataba mlinda lango Farouq Shikalo na Ally Mtoni 'Sonso' huku pia ikelezwa kuwa tayari wamempa mkataba Metacha Mnata
Utata umebaki wa Gadiel ambaye anasikilizia nafasi ya kwenda kusakata kabumbu nje ya nchi
Yanga kumgeukia Rutanga
Julai 11 ndiyo dirisha la usajili wa CAF litafungwa hivyo bado upo muda wa Yanga kufikia muafaka na Gadiel
Lakini inaelezwa Yanga inaweza kurejea kwa beki wa Rayon Sport Erick Rutanga ambaye uongozi wa timu hiyo ulishafanya nae mazungumzo
Rutanga ni mmoja wa wachezaji ambao walitarajiwa kusajiliwa na Yanga msimu huu
No comments:
Post a Comment