Usajili huo utafanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya huku ukihusisha mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa na Songwe.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumanne Julai 9, 2019 na Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani ya nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu ieleza shughuli hiyo itakuwa ikifanyika kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 jioni.
“Taasisi itatakiwa kuwasilisha cheti halisi na kivuli chake, stakabadhi ya malipo ya ada ya hivi karibuni, katiba ya jumuiya/taasisi husika iliyopitishwa na msajili, barua inayothibitisha uwepo wa jumuiya hiyo kutoka kwa ofisa mtendaji wa Mtaa/kijiji ofisi ilipo,” alisema Kingu
“Taasisi ambazo zitashindwa kuhakikiwa kwa mujibu wa ratiba ya eneo zitalazimika kwenda makao makuu ya wizara Dodoma kwa uhakiki na iwapo zitashindwa kufanyiwa uhakiki kwa muda uliopangwa zitaondolewa katika orodha ya msajili.”
Awamu ya kwanza ya usajili wa taasisi hizo ulifanyika katika mikoa ya Dar es Salaama na Pwani huku awamu ya pili ikihusisha mikoa wa Morogoro, Dodoma, Singida na Manyara.

No comments:
Post a Comment