Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, mkoa wa Arusha nchini Tanzania, Frida Wikesi anamtaja mzazi huyo leo Jumatatu Juni 1,2019 ni Victoria Tarmo mkazi wa kata ya Mang'ola wilaya ya Karatu, ambaye hakutaka mtoto wake Paulo Qwande kwenda sekondari licha ya kufaulu.
Mzazi huyo alinaswa akimpa rushwa ofisa mtendaji wa kata ya Mang'ola, Petro Ngarikoi ambaye kabla ya kupokea rushwa hiyo ya Sh20,000 alitoa taarifa Takukuru ambao waliandaa mtego uliozaa matunda na mtuhumiwa amefikishwa mahakamani.
Mtoto huyo tayari amepelekwa shule ya Domeli iliyopo Karatu ambayo alikuwa amefaulu kuanza kidato cha kwanza.
Hili ni kati ya matukio machache tu yaliyoripotiwa ya wazazi wa jamii ya wafugaji, kuhonga maofisa watendaji na wakati mwingine walimu wakuu ili watoto wao waliofaulu shule, wasiendelee na masoko ili wachunge ama kuolewa na kuna wazazi wamekuwa wakihonga hadi ng'ombe.
No comments:
Post a Comment