Baada ya jana Juni 30, 2019 shirikisho la soka nchini (TFF), kufungua dirisha la usajili, klabu ya soka ya Simba inaendelea na usajili, ambapo inaelezwa imeshamalizana na kiungo wa Kenya.
Simba ambayo tayari imeshasajili nyota watatu kutoka Brazil, itamalizana na kiungo Francis Kahata, ambaye amemaliza mkataba wake na Gor Mahia.
Kahata akiwa jijini Cairo kwenye michuano ya AFCON 2019, amefanya mahojiano na EATV&Radio Digital, na kueleza kuwa atasaini Simba baada ya fainali hizo.
Francis Kahata
''Bado lakini muda wowote inaweza kuwa hii wiki au baadaye nitasaini mkataba na mambo ya pesa inabaki kuwa siri yangu lakini mkataba utakuwa wa miaka miwili'', ameeleza Kahata.
Kahata anacheza nafasi ya winga wa kushoto na kama kiungo mshambuliaji ambapo katika mchezo wa Kundi C dhidi ya Tanzania alianza.
No comments:
Post a Comment