Mchezo wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini, umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1
Mabao ya timu zote yalipatikana kwenye kipindi cha kwanza Simba ikitangulia kufunga kupitia kupitia kwa Clatous Chama kwenye dakika ya 33 na Mulenga akaisawazishia Pirates kwenye dakika ya 40
Huo ulikuwa mchezo wa mwisho wa kujipima kwa kikosi cha Simba kilichoweka kambi Afrika Kusini tangu Julai 17 2019
Simba imecheza michezo minne nchini humo, ikishinda 4-0 dhidi ya Orbit Tvet, mabao 4-1 dhidi ya Platinum Stars kisha kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Townshoip Rollers
Simba wanatarajiwa kurudi Tanzania kesho Jumatano, Julai 31 2019
No comments:
Post a Comment