Mtandao wa dailymail umeripoti kuwa Chelsea wamemfungia maisha kuingia uwanjani kutazama mechi za Chelsea kwa shabiki wao aliyeonesha vitendo vya ubaguzi wa rangi kwa staa wa Man City Raheem Sterling wakati wa mchezo kati ya Chelsea na Man City.
Raheem Sterling aliingia katika wakati mgumu December 8 2018 katika uwanja wa Stamford Bridge alipokuwa anakwenda kuokota mpira wa kurusha ndipo alipotolewa kelele za ubaguzi wa rangi na mashabiki wa Chelsea hivyo uchunguzi ulianza mapema na kuonesha kama hakuna ushahidi wa kutosha ila Chelsea imefanya uchunguzi wao pia.
Mchezo huo ambao Man City walipoteza 2-0 Sterling alitolewa lugha zisizofaa na wengine walioonesha vitendo hivyo ambao wanatajwa kufikia watano wamefungiwa kwa muda kuingia uwanjani yaani kwa kipindi kisichozidi miaka miwili na mmoja ndio maisha.
No comments:
Post a Comment